Thursday 10 May 2012

ORODHA YA EDU-ENTERTAINMENT PART II ,HABARI ZA LOON & LEGEND KIM & TH E BOYS


1.   Randy’D’Dawn-Msanii chipukizi wa kujitegemea ambaye yupo chini ya lebo ya ASAR ENTTERTAINMENT ambaye anamalizia masomo yake juni mwaka huu Kampala International University(Dar-Es-Salaam,KIU)

RANDY"D"DAWN
2.   INNOCENT SAHANI (D-KNOB)-Msanii wa kujitegemea kutoka lebo ya mitaani most wanted ambaye yupo Kampala International University(Dar-Es-Salaam,KIU).
D-KNOB

3.    STEVE MDOE(STEVE B)-DJ wakutegemewa kutoka clouds FM ambaye anachukua shahada yake ya computer (IT) pale IFM (CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA)
STEVE-B

4.   LAMAR –mtaarishaji wa muziki anayejitegemea na pia miiliki wa FISHCRAB RECORDS. amehitmu elimu ya juu ya computer (Learn-IT).

LAMAR
5.    EDDIE JUMA-CEO wa ILALAZONE na MTAARISHAJI wa VIDEO na FILAMU amehitimu shahada ya juu ya computer (INDIA NA HOLLAND).
EDDIE JUMA

6.    OTHMAN SUKA-ni rapper na pia meneja wa ratiba clouds FM amehitmu Dar es salaam School of Journalist (DSJ).
 
suka


ORODHA ITAENDELEA AWAMU IJAYO ENDELEA KUFUATILIA SWAHILI HIP HOP FAMILY CLUB BLOG(stori na Mtafiti-0688-300081)




JE ULIJUA KUWA LOON ASLIMU NA KUWA  MUISLAM?

Kwa mara nyingi kwenye swahilihiphop-kimataifa tunazo habari za rapper aliyekuwa chini ya lebo BAD BOY loon ,ameushtua ulimwengu baada ya kuamua kuslimu na kuwa muislamu…! sababu za kuchukua hatua hiyo bado hazijajulikana lakini watafiti wako wa swahili hip hop family BLOG wameweza kukupa kionjo cha picha alivyokuwa mwanzo na sasa jionee mwenyewe rapper huyo, duh..bwana loon… mungu akujaalie.lakini kwa mpenzi hip hop huwezi shangaa sana manake pia kumekuwa na mpasuko wa hapa na pale katika lebo ya BAD BOY, sababu sio rapper wa kwanza kufanya hivyo kutoka BAD BOY, pia rapper mwingine mahiri anaye kwenda kwa jina la MASE naye pia aliamua kumfuata Yesu na kuokoka  (born again) vyanzo vyetu bado havielewi hasa wasanii kinachowasibu kwenye lebo hiyo. utasikia kauli hii kutoka kwa mase inarudiwa tena LOON…” mi sipo tena BAD BOY namrudia mungu…, nadhani hilo ndo jibu sahihi… !!”, je BAD BOY kunaupotoshaji ? kuna nini BAD BOY ? au P.Diddy ni Bad Boy wa kisirisiri ? mi na we hatujui ila kaa chonjo na swahilihip-hop blog, pengine tunaweza pata ufafanuzi zaidi siku zijazo.
(stori na Mtafiti-0688-300081)























JE NI WANGAPI WANAMJUA KIM AND THE BOYS ? NA MCHANGO GANI AMETOA KWENYE SWAHILI HIP HOP


ukizungumzia madj na mapromoter wakati wa mwanzo hip hop tanzania inaanza kusikika masikioni mwa wa waswahili uwezi kuacha kumtaja KIM kwa waelewa hili jina sio geni, ni DJ maarufu nchini aliyewahi kutamba katika medani ya muziki jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, Abdulhalim Magomelo ‘Kim & The Boys,’. alijizolea umaarufu jijini dar es salaam na nchini kwa ujumla, kwenye miaka ya 80' na 90'.
Kim enzi ya uhai wake kwenye harusi yake
Wapenzi na mashabiki wa burudani wa zamani, wataukumbuka mchango wake katika muziki na ucheshi wake, Kim ni Dj aliyewika vilivyo kwa umahiri wa kazi yake katika madisko mbalimbali jijini Dar es Salaam kama Mbowe Disco, na Silver Sands Disco miaka hiyo. Vile vile Kim ni muasisi wa shindano la Yo-rap Bonanza.kwa hivi sasa bwana kim ni marehemu,
Kwenye mazishi na shughuli nzima ya msiba watoto wote wa mjini walikuwepo, vijana wazamani, kuanzia wanamuziki wa kizazi kipya, ma Dj wa zamani na wapenda burudani wote.
Kim ndiye aliyeyatoa majina kama Black Moses (RIP), Ommy Sidney , Othman DigaDiga, Saleh Jabir, II Proud (Sugu / Mr II) pamoja na wengine wengi.

kim akizikwa mnamo tarehe 17th december 2009 kisutu dar es salaam (R.I.P)

kim akiwa na washkaji zake wa kwanza kulia akifuatiwa na ebony maalim,msahbiki na samia-x
Kim ambaye alifariki kwa maradhi ya moyo.hatimaye alizikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar Es Salaam jioni ya tarehe 17th December 2009 . 
mungu ailaze pema peponi roho yake AMEEN.



No comments: