SOMA HABARI HII HALAFU NA RUHUSU MALUMBANO JUU YA UTAMADUNI HUU : Sir Andy Chande Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons
*Nimepata
kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za
utuwema na ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu
mawazo yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki
kwangu katika Freemason
SIR ANDY CHANDE |
*Mwaka
1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa
zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afrisa Mkuu wa Wilaya wa
kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule Nairobi ambao
wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane
katika Afrika nzima
*Freemason Tanzania wamesaidia kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama Theresa; shule ya
Vipofu ya Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali
ya Mnazi mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni.
Tangu miaka hiyo ya 1920 idadi ya vikundi vya Mason nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla imeendelea kuongezeka. Ogezeko kama hilo hilo limejidhihirisha katika Asia, Marekani ya kusini,
na baadaye Ulaya ya Mashariki, baada ya kipindi kile cha kuingia kwa
ukomanisti lakini kwingine kote hasa Ulaya ya Magharibi, Amerika ya Kusini
na Australia, idadi ya Wanachama wa Mason wamekuwa wakipungua polepole
na kuacha pengo kubwa duniani kutoka milioni saba waliokuweko wakati
wa vita kuu ya kwanza hadi kufikia milioni tano tu.
Hata
hivyo mchango wanaodai kuutoa ndugu hao millioni tano, kwa Chama chao
na kwa Jamii, ni mkubwa sana. Wanatoa misaada kila mwaka, kulingana na
kazi zinazotekelezwa na vikundi vyao, kiasi cha dola milioni 400 za
Marekani. Huku Tanganyika, baadaye Tanzania, walisaidia kituo cha watu
wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama
Theresa; shule ya Vipofu ya
Pongwe, mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi
mmoja kula Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni, ni machache tu kati
ya miradi mingi iliyogharimiwa na vikundi vya Mason.
Kati
ya miradi hiyo yote, ule wa Shule ya Buguruni ndio ninaouthamini sana
moyoni mwangu; maana mimi ndiye mwandishi na mchangishaji mkuu wa
fedha; mhamasishaji na mtetezi mbele ya Viongozi Wakuu kwa niaba ya
shule hiyo kwa muda wa miaka thelathini iliyopita lakini bado pamoja na
shughuli zote hizo za maana, kwa muda wote huo niliokuwa Mwanachama wa
Freemason mara nyingi wale Wanachama wa Zamani wamenyanyaswa sana na
magazeti ya nchi za Magharibi.
Kutoka
kuonekana kuwa Chama ambacho huruma na dhamiri zake katika kumwinua
binadamu zinathaminiwa, kama ilivyokuwa katika kipindi kirefu cha karne
za kumi na nane na kumi na tisa na mwanzo wa karne ya ishirini, sasa
kimeporomoshwa hadhi kw amashambulizi makali ya magazeti yasiyokuw ana
msaada, kiasi cha kuigeuza Freemason kuwa kama kivuli tu, kikundi cha
wafitini cha ajabuajabu waliojaa hila
SIR CHANDE NA RAIS MSTAAFU MKAPA |
Ili
kuanza kukielewa vizuri zaidi Chama hiki, na hivyo pengine kuanza
kuoanisha dhana na hali halisi, lazima mtu arudi kwenye misingi
Freemason itikadi yenyewe ya Wema na maadili ndiyo ilivyonitumbukiza
katika mazungumzo yangu ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1950 na akina
Campbell Ritchie na Maclean, juu ya huruma kwa binadamu. Wakati ule
ndipo nilipoanza kutambua kuwa, kumbe, maana kamili ya Uanachama wa
Freemason ni Sayansi ya Maisha ambayo lengo lake ni kumtia moyo
mwanadamu kwa kumwelekeza vile anavyotarajiwa kuwa mtu mwenye ukamilifu katika vyote.
Sehemu kubwa ya hoja hiyo ya Ukamilifu wa mtu inafichwa katika dhana, na pengine
ndiyo maelezo ya uvumi unaoelekezwa kwenye shughuli za Freemason.
Lakini taratibu hizo zimejengwa kwa malengo ya makusudi, ambayo mimi
nayaona kuwa mazuri tu, ya kuamua na kuboresha fikra, moyo na hadhi ya
binadamu kwa hiyo katika hatua ya kwanza ya kuingizwa kwenye Freemason,
mising mkuu ya maadili ya kusema kweli inayojenga Freemason
inasisitizwa kiasi cha kutosha katika mawazo ya mtu anayetaka kujiunga
na Chama au mtahiniwa.
Hatua
ya pili ya Freemason inasisitiza kuendelezwa kwa vipaji na ufundi
katika sanaa na sayansi ili mtu aweze kuwa na manufaa makubwa kadiri
inavyowezekana katika maisha. Hatua ya tatu inatoa nafasi kwa mtu
kufikiria saa chache za mwisho wa maisha yake, lau kama hili litaonekana
kuwa kama ndoto kwa njia hivyo, huyo anayetaka kujiunga na Freemason
anaelekezwa namna ya kuishi kwa kutumia nafasi zote kabisa zilizopo
katika namna inavyooana na misingi mitatu ya Freemason, ambayo ni:
Upendo wa kindugu, misaada na ukweli, na kwamba kifo ni lazima.
Misingi
ni mitatu ikisha kufafanuliwa katika malekezo ya wakufunzi
yanayositiri mengi kati ya matunda ya Freemason, ndiyo ilivyovutia
zaidi nilipopata kujua kwa ndani, kwa mara ya kwanza, baadhi ya mambo
katika kikosi cha Antient. Katika taratibu za Freemason, mzingi wa
upendo wa kindugu unawaelekeza ndugu zetu wote kuwatambua binadamu
wote kuwa familia moja iliyoumbwa na huyo Mwenyezi, lakini wakati huo
“msaada” unatoa ujumbe kuelekeza imani niliyofunzwa na baba yangu,
yaani kuwasaidia wenye shida iwe katika kuwapunguzia umasikini, au kuwaliwaza wanaosumbuliwa na matatizo. Huo ni wajibu wetu sisi sote.
“Ukweli”,
msingi wa tatu nap engine, ndio muhimu kuliko yote ni dhana takatifu
ambayo, kwa mwanachama wa Freemason, ndio msingi wa kila jema la
binadamu “kuwa mtu mwema na kweli” ni somo linalotolewa mapema kwa kila
mtu anayetaka kuingia katika Freemason; hivyo ni kauli inayotumiwa kila
mahali kama zana ya kurekebisha na, kama ikibidi kuelekeza njia ya
maisha na vitendo vya mtu kulingana na masharti yale manne muhimu ya
Freemason: kiasi, uvumilivu, busara na haki.
Na
misingi yote hii, na maadili na umuhimu unaojumuisha siyo tu mafunzo
ya falsafa za watu wa kale, kuanzia wagiriki, paka Budha, mpaka
Zaroster. Lakini hata za dini zinazojulikana. Kinyume na propaganda
zinazoenezwa za Mafashisti wa kiitaliano na wengine wengi zaidi ya hao,
Freemason si chombo cha dini wala vile vile, kinyume chake, hakipingi
dini; kwa kweli Freemason wanawakaribisha watu wote bila kujali imani
zao za dini, wala hawafanyi mbinu za kubadili imani zao wala kuelekeza
ibada zao; wanachojaribu tu ni kuwafanya binadamu bora zaidi.
FREEMASONS WAKIWA KWENYE SHUGULI ZA KIJAMII |
Hivyo
hiyo ndiyo dunia niliyoitumbukia mwaka 1954, na ikawa sehemu muhimu ya
maisha yangu kuanzia hapo. Katika kipindi hicho nimepata bahati ya
kushuhudia kujitolea kwa Wanachama wa Freemason katika kuwasaidia wenye
shida ndani ya Afrika Mashariki na hata nje ya hapo. Nimepata kutambua
umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utuwema na
ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu mawazo
yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu
katika Freemason; na kuimarika huko kunatofautiana kabisa na hisia
zinazotangazwa katika magazeti mashuhuri ya nchi za magaribi. Kuwasaidia
wenzetu kuwasaidia wengine ndiyo misingi niliyojifunza katika miaka
yangu mingi ndani ya Freemason.
Baada
ya kushika nafasi za juu zaidi katika kambi hii ya Nyota ya Jaha mnamo
miaka ya mwisho wa 1950 na 1960 nikateuliwa kuwa kiongozi mstahiki
mwaka 1967, wakati huo ndio kwanza nimeteuliwa Rais wa Muungano wa
vyama vya Round Table vya Afrika Mashariki.
Mwaka uliofuata, kwa vile nilivyokuwa Mwanachama wa kwanza wa Round
Table asiyekuwa Mzungu, nikawa raisi wa kwanza wa Roundi Table na vyama
vinavyoambatana nayo duniani mwenye asili isiyokuwa ya kizungu: ukweli
ulioinua hadhi ya nafasi hii kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko
ilivyokuwa kawaida.
Kwa
nafasi hiyo nikalazimika kusafiri sana, kuandamwa na Magazeti, na kuwa
na shughuli nyingi za uwakilishaji kimataifa, mwaka 1970 nikakamilisha
kipindi changu cha uongozi kama rais wa Kimataifa wa Baraza la Dunia
la Klabu ya Huduma za Vijana; na mwaka uliofuata, baada ya kulazimika
kustaafu kutoka katika chombo hicho kwa sababu ya umri, nikiwa makamu wa
kudumu (wa heshima) wa Mwenyekiti wa Muungano wa Round Table katika
Afrika Mashariki mwaka 1970 nikajiunga na Round Table ya Dar es salaam,
hatua ya kwanza kuelekea kwenye nafasi ya Gavana aliyewajibika na klabu
sabini na nane katika sehemu kubwa ya Afrika.
Mwaka
1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa
zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afrisa Mkuu wa Wilaya wa
kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule Nairobi ambao
wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane
katika Afrika nzima.
Kila
nilivyopata madaraka makubwa zaidi, ndivyo nilvyohakikisha kwamba
nilifanya kila lililowezekana kutakasa Freemason mbele ya Umma. Kwa
uzoefu wangu mimi, watu kwa kawaida hutilia mashaka, na hata kuogopa,
mambo wasiyoyaelewa. Kwa hiyo wakati wote nilipoulizwa habari za
Freemason nikajitahidi kumweleza huyo muulizaji misingi ya chombo hicyo,
nikisisitiza kwamba hakikuwa chama cha siri, na wanachama wake
wanajulikana wazi: na kwamba mikutano yake haifanyiki katika sehemu za
kujificha ila katika kumbi za mikutano zinazojulikana, zenye hati ya
serikali na zinazoweza kutambulika wazi wazi.
Kama
nilivyokwisha kusema mapema chama hiki na maajabu yake, kiliingia
wakati wa Vita Vikuu vya pili, tulipokuwa tunajaribu kuwalinda wanachama
wetu waliokuwa Italia, ufaransa na Ujerumani dhidi ya vituko vya
mataifa makubwa toka wakati huo tumejidhihirisha wazi wazi mbele ya
umma, na kujitahidi wakati wote kuwaondolea mashaka na kudhihirisha kuwa
chama chetu ni chombo kinachomwingiza mtu mwema na kujitahidi kumfanya
mwema zaidi.Habari yote hii ni kwa Mujibu wa kitabu cha Sir Andy
Chande.
LAKINI BADO WASWALI YAPO MENGI TU KUHUSIANA NA DINI HII NAOMBA COMMENTS ZENU.
No comments:
Post a Comment