Thursday, 3 May 2012

GNL-ZAMBA LUGA-FLOW M.C ALIYEWEKA HISTORIA NA MSOMALI KNAAN


Unaposema hip hop ya east africa uwezi kuacha kumzungumzia mtu anayeitwa GNL ZAMBA ni M.C kutoka Uganda..., basi bila shaka huyu jamaa sio mgeni masikioni mwenu, mnamo 2010 kipindi hicho africa kusini inaweka historia pia kwa bara zima la africa,yani kuwa mwenyeji wa kombe la dunia... basi yeye aliweka historia yake ya kufanya track na knaan mmarekani mwenye asili ya Somalia hivyo basi.., ni uzoefu gani alipata kutoka kwa knaan., nasi tujifunze nini?  hii nyimbo inaitwa “Orchestra” kibao hiko kilicho sheeni utaarishaji wa hali ya juu kilimfanya gnl apagawe na kusikia ushindi faraja moyoni mwake.kwa GNL ilikuwa ni ndoto ya kweli.
GNL-ZAMBA
KNAAN
K’NAAN amekuwa maarufu sana kimataifa na  wimbo wake wa "Waving flag" kipindi cha kombe la dunia.huo wimbo na knaan umempa nguvu ya kutangaza luga-flow nchini Uganda.

“Mikataba ya kueleweka ndio njia pekee ya kuzungusha gurudumu la maendeleo ya hip hop” ndivyo alivyokuwa akisema GNL Zamba. hivyo basi nasi kama we wahangaikaji au we wanaharakati shikilia ndoto yako amini unachokifanya GNL kaamini amefanikiwa hatua moja kwenda nyingine.umuhimu wa kufanay kolabo ni kongeza mashibiki na pia kuborehsa sanaa yako....., wasauzi wanasema "amandraa" na waswahili wanasema "tusonge".
                                

No comments: