Monday, 30 April 2012

MAPINDUZI YALIFANYIKA MWAKA 2007 WALIPOTUA DEAD PREZ SWAHILI-LAND


Mwaka 2007 ulikuwa ni mwaka wa faraja kwa wanaswahili hip hop nchini ,ni kipindi walipotua hip hop icons toka marekani DEAD PREZ pengine wengi wenu hili kundi ni geni maskioni mwenu lakini kwa wanahip hop wa miaka 90’ wanalitambua vizuri sana..DEAD PREZ walitua nchini kwa udhamini wa BIRITSH COUNCIL, hapo tunaweza sema ndio mapinduzi ya kwanza na yakweli kutoka kwa wasanii  nchini Tanzania, mapinduzi hayo yalifanywa na waasisi kutoka kundi bora la Swahili hiphop nchini TANZANIA ,KWANZA UNIT ndio…hakuna pingamizi juu ya hilo…likiongozwa na kiongozi wao Rhym-son au Chief Rhymson au Zavala pamoja na mwenzake Kibacha au K-Singo au KBC , Dead Prez waliongozwa na M-1 na Umi. dhumuni la ujio huo ulikuwa ni kuwapa  tumaini na kuhamasisha utamaduni na mwendo mzima wa hip hop nchini (Swahili hip hop) na tunajifunza nini ukilinganisha na mwenendo wa kwao marekani.. kilichogundulika ni kwamba swahili-land tunarasilimali za kutosha katika Nyanja nzima ya Swahili hip hop.


M-1 na Umi wanaounda kundi la DEAD PREZ kutoka marekani wakilianzisha na mapinduzi ndipo yalipoanza.
 
kuhusu kujifunza nilipata mahojiano na mkongwe wa swahili hip hop Imam Abbas hiki ndicho alichojibu” uumh…kwanza nimefurahi sana kuja kwa icons hawa ila pia napenda kuwakumbusha wapenzi wa swahili hip hop waelewe hili jambo tayari tunaandika historia ,kwamba wasanii wenyewe wameamua kuwaleta wanamapinduzi wenzao ni kama miujiza bigup to kwanza..ha ha ha kweli wao ni wa kwanza saluti, pili kushusu kujifunza na ujio wao kwanza wanajikubali kwamba wao ni wenzetu..na usaidizi unakuja wa kiitifaki zaidi ilikuboresha nguzo za hip hop kama mavunjo (breakdance),sanaa za kutumia mikono (grafitti)na zingine na pia kuwashawishi wadhamini watambue na waelewe hip hop ni tamaduni kama zingine kwa hilo nawapongeza Dead Prez .tatu waliokuja nayo sio mengi na sio mageni sababu sisi tulianza sikiliza hip hop tangu mwaka 1989 hivyo basi kikubwa sisi tunachokata ni connection tu za kupata record contract za kueleweka na kupata utambuzi kwenye asasi za kiserikali na zisizo-za-kiserikali ilikusonga mbele kama alivyo sema M-1, sababu tofauti yetu na wao ni lugha sisi kughani  Kiswahili na kiingereza wao kiingereza tu..,lakini tumejifunza sababu mtu hawezi toka mbali halaf usijifunze kitu itakuwa uongo….BIG UP DEAD PREZ…!!!”  


M-1 namiondoko ya kujigamba BRITISH COUNCIL.

Umi akishangaa watu walivyojitokeza  BRITISH COUNCIL.

Umi akibadilishana mawazo na mkali wa ragga nchini Zanzi-B.
Mkongwe KBC akiwa na Chidi Benz ,Kurasa ,Fid-Q na Lindu anachukua vipande vya luninga.

MAVUNJO pia yalikuwapo USIPIME.......

mdogo wake marehem D-Rob JLT pia akichukua vyake huku KURASA akinyoosha kidole kwa nyuma.

M-1 na shabiki wake.

YEEES..! Hiyo kali..... Umi akiwa na Joh Makini na Chidi Benz.

Na Kauli Mbiu ilikuwa "TUPO-PAMOJA" ndio bwana amani tu.

Usini sahau mi ndio AVERI...bwana(t-shirt nyeusi).
heavy weight M.C Prof.Jizzy na mshabiki wake.

KBC akilianzisha kulia kabisa Imam Abbas Fid-Q na Kurasa.

Tafakuri Mgavi Dosi Dr.Eibbas ,Adili na Kalapina wote ndani ya nyumba.

Lets Keep It Swahili Kati Kulia Zavala na Evans Bukuku.

Man-suli Akiwakilisha.

Randy'D'Dawn na mshabiki wake pia alionyesha luuuv...

Jamani na mie nimo...ha ha ha Mchomvu baby.....

SAIGON kalinye.. kalinye... kalinye oi oi oi oi....!!!!....oi oi mchomvu akisikilizia.

Dada yetu Enika hakuwa nyuma pia ndni ya nyumba.

We Mejah..!! umemaliza kazi manake bila ya wewe hapo mambo yote yameharibika..cheka kidogo ha ha ha ha pamoko sana.

Event Meneja wa Swahili hip hop family club LOCAL kati akijiachia na Prof.Jay na K-wa-Mapacha.

Ulidhani Rock City itakosa wewe....!! ,umejidanganya RADO Hapa.........!!!

No comments: